Wanafunzi 35 wa Chuo Kikuu watekwa nyara Nigeria
22 Septemba 2023Watu waliojihami kwa silaha nchini Nigeria wamewateka watu 35 kutoka chuo kikuu cha kaskazini-mashariki mwa Zamfara siku ya Ijumaa, katika tukio kubwa la utekaji linalowahusisha wanafunzi mwaka huu.
Magenge ya silaha yameshamiri katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, yakiteka watu kwa ajili ya kikomboleo, kupora na kuharibu jamii na kuwaua raia.
Majaribio ya vikosi vya usalama kusitisha ghasia za makundi hayo yamekuwa na ufanisi mdogo.
Msemaji wa gavana wa Zamfara, Mugira Yusuf, amesema wanafunzi 24, wafanyakazi 10 na mlinzi walitekwa na watu wenye silaha mapema Ijumaa, kutoka chuo kikuu cha shirikisho cha Gusau.Wabeba silaha waua 3, wawateka 20 chuoni Nigeria
Utekaji wa wanafunzi, ambao zamani ulikuwa unatumiwa na makundi ya wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu kuwatishia raia, umegeuka kuwa sekta ya kuchuma pesa na magenge ya uhalifu yanayoomba fidia.