Wanachama wa NATO watakiwa kuitikia wito wa Ukraine
19 Aprili 2024Matangazo
Ujerumani imezitaka nchi wananchama wenzake wa NATO kupeleka mifumo ya ulinzi wa anga inayohitajika mno nchini Ukraine, ikiwemo betrei za ziada za makombora ya Patriot.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya njini Brussels Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema, hakuna sababu ya msingi kwa nchi wananchama wa NATO kukataa maombi ya dharura ya mifumo saba ya ulinzi wa anga ya Patriot kutoka Kyiv. Tayari Berlin imeahidi Kyiv kutoa moja ya mfumo huo.
Soma pia:Zelensky ataka NATO kujadili ulinzi wa anga wa Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuomba msaada zaidi wa kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi kamili wa Urusi, kwenye mkutano wa mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya unaonuwia kujadili mzozo huo.