Walinzi wa pwani wa Japan, Korea Kusini wafanya luteka
6 Juni 2024Hatua hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa baharini wa nchi hizo katika kukabiliana na kuongezeka kwa kile zinachodai ni kitisho cha China katika kushinikiza madai yake ya kulidhibiti eneo hilo.
Soma pia: Philippines, US launch annual joint military drills
Luteka hizo zilihusisha meli ya doria kutoka kila nchi na helikopta mbili zilijiunga kwenye pwani ya kaskazini ya Maizuru katika mkoa wa Kyoto. Luteka za pamoja za Alhamisi zilifuatia makubaliano ya viongozi wa nchi hizo tatu Agosti iliyopita ili kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kulinda amani na utulivu katika eneo la Indo-Pasifiki.
Makabiliano kati ya meli ya walinzi wa pwani wa China na Ufilipino yameongezeka katika Bahari ya Kusini ya China, na kusababisha hofu kwamba migogoro hiyo huenda ikaijumuisha Marekani, mshirika wa muda mrefu wa Ufilipino.