Wako wapi wasichana waliotekwa na Boko Haram?
14 Oktoba 2014Juhudi za walimwengu kudai wasichana hao waachiwe huru mpaka sasa hazijaleta tija. Philipp Sandner ameandika kuhusu hofu waliyo nayo wanafunzi wa kike nchini Nigeria,miezi sita baada ya Chibok.
Kauli ni moja tu: "Warudisheni binti zetu. "Bukky Shonibare wa vuguvugu la "Turudishieni binti zetu" au kwa kiingereza"Bring Back Our Girls,machozi yakimchirizika anawaomba,anawasihi na kuwashika miguu anasema Boko Haram wawaachie huru wasichana hao.Uso wake umejaa huzuni,hofu na wasi,miezi sita tangu wasichana hao zaidi ya 200 walipotekwa nyara katika mji wa kaskazini wa Nigeria Chibok hatima yao haijulikani .
Daima Boko Haram wamekuwa wakihujumu vituo vya elimu:pekee katika jimbo la kaskazini la Borno,ngome ya wanamgambo hao wa itikadi kali,wmeshauwa tangu mwaka 2011 zaidi ya walimu 70 na kuvunja shule zisizopungua 900.
Tangu April 14 mwaka huu wa 2014,uvumi ulizagaa vikosi vya usalama vinajua wapi wasichana hao wamepelekwa.Ndio mana wanaharakati wa vuguvugu "Warejesheni binti zetu" wamezidi kughadhibika na kuikosoa serikali kutofanya lolote kuwaokoa watoto hao.
Serikali ya rais Goodluck Jonathan inakosolewa pia na jumuia ya kimataifa.Ili kutuliza lawama hizo serikali imetangaza mradi wa "shule salama" utakaoagharimu dala milioni 100 za kimarekani.Lakini wanaharakati wa vuguvugu la "Warejesheni binti zetu" wanahisi kabla ya wasichana hao kuachiliwa huru hawawezi kuzungumzia kuhusu mradi wa shule salama.Nae Aisha Muhammad Garga ambae binafsi ni mwanafunzi anasema: "Sioni hatua zozote za maana za usalama ktika shule yetu.Serikali inabidi iwapatie silaha walinzi wa shule pia.Hilo likifanyika tu ndipo nitakapoweza kujisikia salama na kuweza kusoma."
Serikali inaonyesha kugutuka.Katika shule ya Mubi katika jimbo linalozongwa na vitisho vya Boko Haram,na Adamawa,walinzi wanapiga doria shuleni ingawa bila ya silaha.Mtaalam wa masuala ya usalama Kabiru Adamu ana shuku kama serikali inaweza kuzilinda ipasavyo shule zote nchini humo.
Mwandishi:Sandner Philipp
Tafsiri:Hamidou Oummilkheir
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman