1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi Ujerumani: Kina Jaafar, Merkel na kukimbia Syria

Saleh Mwanamilongo
27 Agosti 2020

Miaka mitano iliyopita Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikubali kuwafungulia milango wakimbizi kuingia Ujerumani. Familia ya Jaafar iliwasili Berlin mwaka 2015 inategemea kauli ya Merkel katika kuboresha maisha yao.

https://p.dw.com/p/3haB2
Berlin-Mitte Bergstraße "Wir schaffen das" an Hauswand
Picha: DW/C. Strack

''Baba, unanitia aibu kweli!'' Rema na Roshen wamekodoa macho wakati baba yao anapocheza musiki wa Kijerumani. ''Napenda sana Nenas '99 Red ballons'', anajibu kwa kutabasamu baba yao mwenye umri wa miaka 44. Binti zake wana miaka 11 na 12, wanacheza kupitia app ya TikTok muziki wa Kiingereza.

Alipowasili nchini Ujerumani miaka mitano iliyopita Mohammad hakuwa anajuwa maneno ya nyimbo za Nena mwanamuziki maarufu wa Kijerumani wa muziki wa iana ya Pop mnamo miaka ya themanini.

Yeye na mke wake Roka, pamoja na binti zao walikimbia vita jimboni Aleppo, nchini Syria na kuwasili Berlin kupitia Bahari ya Mediterania na barabara za nchi za eneo la Balkan.

Soma pia: Sera ya wakimbizi ilivyoijengea Ujerumani sifa nje

Mohammad alisema kwamba Tulika watoto wetu waishi katika usalama. Mwaka 2015, takribani watu milioni moja waliomba hifadhi kama wahamiaji nchini Ujerumani. Wakati huo Kansela Angela Merkel aliwambia raia wa Ujerumani, wakimbizi na hata yeye mwenyewe kwamba ''Tunaweza'' kuwapokea wakimbizi.

Matamshi hayo yanaivutia familia ya Jaafar hadi leo, lakini yanawaonyesha pia ukomo wao. Tulipokutana kwa mara ya kwanza na familia ya Jaafar mwaka 2016, wakati huo Roshen alikuwa na umri wa miaka minane, na alikuwa na mtizamo mzuri kuhusu Ujerumani.

Wakati huo alikuwa akisema kila kitu ni kizuri Ujerumani, hakuna kitu kibaya hata kimoja. Tayari anazungumza Kijerumani na anawatafsiria wazazi wake. Lengo lake ni kwamba wajihisi kama kwao na waishi kwa furaha.

Soma zaidi: Maoni:Ujerumani haitaweza kuubeba mzigo wa wakimbizi

Roshen na dada yake walimuandikia barua Kansela Merkel na kusema wanataka wazazi wao waenda shule na wawe na nyumba na gari, na wapate ajira na vilevile apate ndugu yake wa kiume.

Deutschland Tausende demonstrieren vor dem Kanzleramt für Grenzöffnung
Maandamano yakifanyika mbele ya ofisi ya kansela mjini Berlin kushinikiza kufunguliwa kwa mipaka kwa wakimbizi kufuatia hali ngumu nchini Ugiriki wanayokabiliana nayo wakimbizi nje ya mipaka ya Ulaya.Picha: Imago-Images/J. Große

Miaka minne baadae, hivi sasa Roshen mwenye umri wa miaka 12, mwaka huu yuko kwenye shule ya sekondari. Roshen anasema anataka kusomea udaktari na ndoto yake ya kuwa na mdogo wake wa kiume imekamilika. Mwaka wa 2017, Richard alizaliwa na miaka miwili baadae Matilda pia.

Richard tayari anakwenda shule ya chekechea na Matilda kaandikishwa pia. Baba yao, Mohammad amesema kwamba wanatakiwa kujifunza Kijerumani kizuri haraka iwezekanavyo.

Nyumbani watoto hao wanazungumza Kijerumani badala ya lugha yao mama. Lakini miaka mitano baada ya kuwasili mjini Berlin, Mohammad na Roka pamoja na watoto wao wanaishi kwenye kambi ya wakimbizi.

Familia hiyo ya watu sita ina eneo la mita 40 za mraba kwa ajili ya kulala, kufanya kazi, kupika, kucheza na kula.

Eneo hilo halina nafasi kwa ajili ya meza ya kulia, au viti. Watoto wenye umri mkubwa wanafanya mazoezi yao ardhini wakati wadogo zao wanalala. Mbali na hilo kuna vizuwizi kuhusu janga la virusi vya corona.

Aidha, wanavumilia maisha hayo, bila bugudha kwa sababu kurejea Syria sio suluhisho. Kigumu kwa familia ya Jaafar ni kuelewana na watu wengine wapatao mia tatu wanaoishi kwenye kambi hiyo ya wakimbizi. Usiku, ni vigumu kulala kwa sababu wengine wanapiga kelele.

Mwaka uliopita hali ya familia hiyo ilianza kuimarika, Mohammad alifanyiwa mtihani wa lugha na alipewa ajira kwenye kampuni ya ujenzi. Lakini miezi minne tu alipatwa na ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis B) na kufutwa kazi baadae.

Soma zaidi: Maelfu waomba hifadhi zaidi ya mara mbili Ujerumani

Toka Januari mwaka huu, Mohammad anapewa mafunzo ya kuendesha basi. Ameahidiwa ajira mara atakapokamilisha mafunzo yake, lakini hivi sasa ana wasiwasi na hajiamini tena baada ya kufutwa kazi mara ya kwanza.

Chanzo: DW