Wahamiaji waliokolewa wakwama kwenye meli za kitalii Malta
3 Juni 2020Wahamiaji zaidi ya 400 wanaendelea kuzuwiliwa kwenye eneo la bahari karibu na Malta,wengi wao kwa wiki kadhaa sasa. Wahamiaji hao waliokolewa kwenye bahari wanahisi kwamba sio raha kubaki muda mrefu baharini bali wanawasiwasi kuhusu hatama yao. Wahamiaji hao ni wale waliookolewa baadhi toka April kutoka meli chakavu za wafanya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.Wanaendelea kusubiri pamoja na serikali ya Malta, nchi ambayo itakubali kuwapokea. Hadi sasa ni Ufaransa pekee imepiga hatua ya kwa kuwakubalia baadhi yao kuingia nchini humo.
Ufaransa ni moja wapo ya nchi za Muungano wa Ulaya zilizokubali mwaka uliopita kugawanya mzigo huo wa kuwahudumia wahamiaji waliookolewa baharini na Malta pamoja na Italia. Lakini maelewano hayo mara nyingi huwa hayatekelezwi. Na hayo ni kabla ya kuzuka kwa janga la Covid-19 ambalo lilisababisha baadhi ya nchi za Ulaya kufunga mipaka yake.
Jumatano shirika la SOS Mediterranee, linalohusika na kuwaokowa wahamiiaji linaeleza kwamba wahamiaji hao wametumiwa kama agenda za kisiasa baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Kwenye mkutano na wandishi habari, waziri mkuu wa Malta, Robert Abela alisema kwamba hali ya wahamiaji hao ni ya kuhuzunisha. Amesema kwamba nchi yake haiwezi kuwapokea wahamiaji hao kwa sababu bandari zake zote saba zimefungwa katika juhudi za kupambana na Corona.
Abela alisema anategemea kuwepo na suluhisho la haraka la Umoja wa Ulaya kuhusu wahamiaji hao. Mwaka uliopita mvutano uliibuka baina ya nchi za Umoja wa Ulaya baada ya serikali ya Italia kusema haitapokea wahamiaji, huku ikizitika nchi nyingine za Ulaya kupokea wahamiaji zaidi.