1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 30 kutoka Afrika wapotea baharini

7 Agosti 2023

Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) linasema wahamiaji wapatao 30 kutoka Afrika hawajulikani waliko baada ya boti mbili kuzama nje kidogo ya pwani ya kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

https://p.dw.com/p/4Uqo6
Mittelmeer Rettungsaktion vor Lampedusa Bootsflüchtlinge
Picha: Italy Coast Guard/ROPI/picture alliance

Shirika hilo limesema manusura wa boti moja kati ya mbili wamesema takribani wenzao 28 wamepotea baharini huku ikiarifiwa wengine watatu kutoka boti ya pili hawajulikani waliko. 

Mkasa huo umetokea baada ya boti hizo mbili kuzama siku ya Jumamosi kutokana na kuchafuka kwa bahari.

Soma zaidi: Watu 57 waokolewa kutoka boti za wahamiaji Lampedusa
MFS: Ufaransa na Italia huwanyanyasa wahamia

Kwenye visa hivyo viwili, mamlaka za Italia zimewaokowa wahamiaji wengine 57 walionusurika baada ya kuparamia mwamba wa mawe baharini. 

Boti zote mbili inaaminika zilianza safari siku ya Alhamisi kutoka mji wa mwambao wa Tunisia wa Sfax.

Uchunguzi tayari umeanzishwa kuhusiana na matukio hayo mawili baada ya polisi kusema walanguzi wanaosafirisha watu huenda walikuwa na taarifa juu ya utabiri wa hali mbaya ya hewa baharini.