1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wanne wa uchaguzi wa rais Tunisia wafungwa jela

6 Agosti 2024

Mahakama ya Tunisia imemhukumu mkosoaji mkubwa wa Rais Kais Saied, Abir Moussi kifungo cha miaka miwili jela, kwa kosa la kuidhalilisha tume ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4j9e3
Tunis | Tunisia | Mkosoaji mkubwa wa Rais Kais Saied, Abir Moussi
Mkosoaji mkubwa wa Rais Kais Saied, Abir Moussi Picha: Chokri Mahjoub/Zuma/IMAGO

Mahakama ya Tunisia imemhukumu mkosoaji mkubwa wa Rais Kais Saied, Abir Moussi kifungo cha miaka miwili jela, kwa kosa la kuidhalilisha tume ya uchaguzi. Abir Moussi ameripotiwa kuwasilisha ombi la kugombea urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 6.

Mahakama pia iliwahukumu jana Jumatatu wagombea wanne waliotarajiwa kuwania uchaguzi wa urais kifungo cha miezi minane jela na kuwapiga marufuku kugombea wadhifa huo kwa mashtaka ya kununua kura.

Wakosoaji wanasema hatua hizo ni mbinu za rais Saied kuwaengua wapinzani wake katika uchaguzi.

Soma pia:Afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tunisia akamatwa

Hapo jana Rais Saied, aliwasilisha fomu ya kugombea urais katika uchaguzi wa Oktoba 6. Saied mwenye umri wa miaka 66 amewaambia waandishi habari mjini Tunis kwamba uamuzi wake wa kugombea urais ni sehemu ya kile alichokiita "vita vya ukombozi" kwa nia ya kuanzisha jamhuri mpya.