SiasaTunisia
Tunisia: Afisa mwandamizi wa chama cha upinzani akamatwa
14 Julai 2024Matangazo
Taarifa ya kukamatwa kwake imetolewa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Taarifa hiyo imeeleza kwamba, Lourimi, alikamatwa bila ruhusa ya mahakama pamoja na wenzake wawili katika mji wa Borj Al Amrim, ulio karibu kilomita 37 kutoka mji mkuu Tunis.
Hata hivyo chama hicho ambacho Mkuu wake Rached Ghannouchi amekuwa gerezani tangu Aprili mwaka jana, hakikutoa sababu yoyote ya kukamatwa kwa Lourimi.
Mwezi Septemba mwaka uliopita, viongozi wawili wa Ennahdha yaani Waziri Mkuu wa zamani Hamadi Jebali na Mondher Ouniss aliyekuwa kaimu mkuu wa chama hicho tangu Ghannouchi alipokamatwa, nao walitiwa mbaroni. Serikali ya Rais Kais Saied ilizifunga ofisi za chama hicho baada ya Ghannouchi kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na ugaidi.