Kongo: Wagombea urais wataka uchaguzi huru na haki
24 Novemba 2023Matangazo
Wagombea hao akiwemo mgombea mkuu wa upinzani Martin Fayulu na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Daktari wa Wanawake Denis Mukwege anayegombea kwa mara ya kwanza, wanadai kuwepo makosa ya makusudi yaliyofanywa na tume ya uchaguzi ambayo yanatilisha shaka uhalali wa daftari la wapiga kura.
Soma pia:Kuondolewa vipeperushi vya wagombea kunazusha mvutano Kongo
Msemaji wa tume ya uchaguzi ya Congo - CENI amekataa kuzungumzia habari hizo.
Mkuu wa tume hiyo katika siku za nyuma alipinga tuhuma hizo, akiliambia shirika la habari la Reuters kuwa tume hiyo itahakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki.