Wafanyakazi Israel wagoma baada ya kuuawa mateka
2 Septemba 2024Mgomo huo unaoanza leo unalenga kupinga namna serikali ilivyoshindwa kuumaliza mzozo baina ya taifa hilo na wanamgambo wa Hamas.
Miji na jamii nyingi zimeunga mkono mgomo huo, ingawa wengine hawakukubaliana nao kwa kuwa ni wafuasi wakubwa wa serikali ya mrengo wa kulia ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Soma pia: Israel inasema imetambua miili sita ya mateka kwenye handaki moja huko Gaza
Jana Jumapili, Histradut ilitangaza kuandaa mgomo mkubwa wa siku moja utakaosimamisha shughuli nchini humo, wakilenga kumuongezea shinikizo Netanyahu, kuingia makubaliano ya kuwaachia mateka waliosalia.
Jeshi la Israel lilitangaza jana kugundua miili sita ya mateka waliokuwa wamefukiwa kwenye mahandaki kusini mwa Gaza na kudai waliuliwa na wanamgambo wa Hamas.
Hamas imekanusha kuwauwa mateka hao.