Wafanyabiashara wa Haiti walilia kuchelewa polisi wa Kenya
18 Aprili 2024Katika barua iliyotumwa kwa Rais William Ruto wa Kenya, viongozi wa mabaraza manane ya juu ya biashara wamesema wana wasiwasi kwamba kikosi cha polisi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya bado hakijapelekwa zaidi ya miezi sita baada kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa, huku muda ulioafikiwa ukikaribia kuisha.
Soma zaidi: Haiti hatimaye yaunda rasmi Baraza tawala la mpito
Kenya, ndiyo nchi pekee iliyojitolea kuongoza ujumbe huo, lakini kufikia mwezi Machi ilikuwa bado haijawasilisha barua kwa Umoja wa Mataifa kuelezea rasmi mchango wake.
Haya yanajiri huku magenge yenye silaha yakizidisha mashambulizi yao katika sehemu za mji mkuu, Port-au-Prince.
Bandari imefungwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, hali inayozuia usambazaji wa chakula na bidhaa muhimu huku mamilioni wakikabiliwa na njaa.