1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waendesha mashataka Georgia kuchunguza matokeo ya uchaguzi

Josephat Charo
30 Oktoba 2024

Afisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa Georgia imesema hivi leo kwamba inaanzisha uchunguzi wa uwezekano wa udanganyifu katika uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumamosi iliyopita.

https://p.dw.com/p/4mOQ1
Bendera ya Gerogia na EU
Bendera ya Gerogia na EUPicha: Zurab Tsertsvadze/AP/picture alliance

Afisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa Georgia imesema hivi leo kwamba inaanzisha uchunguzi wa uwezekano wa udanganyifu katika uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumamosi iliyopita, ambapo chama tawala cha Georgian Dream kilipata wingi mkubwa kwa kura ambao upinzani ulisema ni udanganyifu.

Afisi ya mwendesha mashtaka mkuu imesema rais wa Georgia Salome Zourabichvili, mkosoaji wa serikali ambaye amekosolewa mara kwa mara akisema kulifanyika udanganyifu katika uhesabuji wa kura, ataitwa kuhojiwa katika uchunguzi huo siku ya Alhamisi.Georgia yajiandaa kwa maandamano baada ya kura

Waangalizi wa uchaguzi wakiwamo wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE lenye nchi 57 wanachama wamesema uchaguzi wa Georgia uligubikwa na matukio ya vitisho, rushwa na kura zisizo halali kuingizwa katika masanduku ya kupigia kura, hali ambayo huenda iliathiri matokeo ya uchaguzi. Waangalizi hao hata hivyo walisita kusema matokeo ya uchaguzi huo yalichakachuliwa.