1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Georgia awataka raia kupinga uchaguzi wa bunge

28 Oktoba 2024

Rais wa Georgia amesema hayatambui matokeo ya uchaguzi wa bunge, ambao maafisa wa uchaguzi wanasema chama tawala ndicho kilishinda. Rais Salome Zourabichvili amesema nchi yake ni mwathiriwa wa operesheni maalum ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4mIJp
Uchaguzi Georgia | Rais Salome Surabischwili
Rais Salome Surabischwili anasema Urusi inataka kuwazuia kujiunga na Umoja wa UlayaPicha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance

Rais Salome Zourabichvili amesema nchi yake imekuwa mwathiriwa wa kile alichokiita "operesheni maalum ya Urusi" iliyolenga kuiondoa kwenye mkondo wa kueleka Ulaya.

Akisimama pamoja na viongozi wa upinzani, Bi Zourabichvili aliwahimiza raia wa Georgia kuandamana Jumatatu usiku katika barabara kuu ya mji wa Tbilisi kupinga kile alichokiita uchakachuaji wa matokeo na wizi wa kura zao. Hatua hiyo inaongeza uwezekano wa msukosuko wa kisiasa katika taifa hilo.

Soma pia: Georgia yafanya uchaguzi wa bunge

Amezungumza siku moja baada ya kufanyika uchaguzi ambao huenda ukaamua kama Georgia inataka kujiunga na Ulaya au itaanguka kwenye ushawishi wa kujiunga na Urusi. Tume ya Uchaguzi ilisema kuwa chama tawala cha Georgian Dream kilishinda kwa 54.8% ya kura wakati muungano wa vyama vinne vya upinzani vinavyopigia upatu Umoja wa Ulaya, ukiibuka na asilimia 37.58%.