Walinzi wa Rais Yoon wawazuwia wachunguzi kumkamata
3 Januari 2025Tukio hilo ni la karibuni katika mgogoro wa kisiasa ambao umezikumba siasa za Korea Kusini na kushuhudia wakuu wawili wa nchi wakiondolewa madarakani katika kipindi cha mwezi mmoja.
kuwazuia kwa saa kadhaa kuingia katika makazi ya Yoon, kutokana na wasiwasi kuhusu usalama wao.
Limesema wapelelezi wake walisukumana na vikosi vya usalama wa rais. Nje ya makazi ya rais, idadi kubwa ya waandamanaji wanaomuunga mkono Yoon walivumilia baridi kali kwa saa nyingi, wakipeperusha bendera za Korea Kusini na Marekani na kuapa kumlinda.
Polisi ya taifa imesema inapanga kuanzisha uchunguzi dhidi ya mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais na manaibu wake kwa tuhuma za kuzuia utekelezaji wa majukumu ya polisi, na imewaita ili kuhojiwa kesho Jumamosi.
Soma pia: Maafisa Korea Kusini wajaribu kumkamata Rais Yoon
Zaidi ya maafisa 200 wa ulinzi wa rais na wanajeshi waliunganisha mikono ili kuwazuia wachunguzi na polisi . Afisa mmoja amesema kuwa licha ya kushuhudiwa matukio ya upinzani, hakuna yeyote aliyetoa silaha.
Yoon, ambaye amejifungia ndani tangu alipoondolewa madarakani na bunge mnamo Desemba 14, hakuonekana wakati wa purukushani hizo.
Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema wanajeshi wako chini ya kitengo cha Ulinzi wa Rais. Shirika la Kupambana na Rushwa limesema litatafakari hatua zaidi za kuchukuliwa.
Chimbuko la madhila ya Yoon
Wapelelezi wa rushwa wanatafakari kumfungulia mashtaka ya uasi baada ya Yoon, aliyedai kuwa sera zake zinapingwa na bunge lililotawaliwa na wawakilishi wa upinzani, kutangaza sheria ya kijeshi Desemba 3 na akawatuma askari kulizingira bunge.
Bunge lilibatilisha amri hiyo kwa kauli moja ndani ya saa chache na likamvua Madaraka mnamo Desemba 14 likimtuhumu kwa uasi.
Maafisa wa kupambana na rushwa na waendesha mashitaka nao wakaanzisha uchunguzi tofauti kuhusiana na matukio hayo.
Mahakama ya mjini Seoul ilitoa waranti wa kumkamata Yoon na waranti mwingine wa kuyapekua makazi yake, lakini kuzitekeleza hati hizo ni vigumu kwa sababu rais huyo amejifungia katika makazi yake rasmi.
Soma pia: Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini kuamua hatma ya Rais Yoel
Mawakili wa Yoon, waliowasilisha jana mahakamani kesi ya kupinga hati ya kukamatwa kwake, wanasema haiwezi kutekelezwa katika makazi yake kutokana na sheria inayolinda maeneo yanayohusishwa na siri za kijeshi dhidi ya kufanyiwa upekuzi bila ya ridhaa ya mtu anayehusika.
Waranti wa kukamatwa Yoon ulikuwa wa wiki moja tu kwa hiyo utamalizika muda wake Januari 6.
Mawakili wa Yoon pia wanahoji kuwa Shirika la Kupambana na Rushwa, linaloongoza uchunguzi Pamoja na polisi na jeshi halina mamlaka ya kuchunguza madai ya uasi.
Aidha, wamesema polisi haina mamlaka ya kisheria ya kusaidia katika kumkamata Yoon, na wanaweza kukamatwa na kitengo cha ulinzi wa au raia.