Wachezaji wa Germany watapokea Euro elfu 50 kutoka kwa DFB
24 Juni 2024Bao la dakika za lala salama la Ujerumani lilofungwa na Niclas Füllkrug na kupelekea sare ya 1-1 dhidi ya Uswizi mwishoni mwa juma limewafanya wachezaji wa timu hiyo ya taifa kupokea bonasi yao ya kwanza ya malipo kwenye mashindano ya Euro 2024 yanayoendelea.
Soma zaidi. Ujerumani yawa ya kwanza kufuzu duru ya mtoano
Kila mmoja wa wachezaji 26 atapokea Euro 50,000 kutoka kwa Shirikisho la Soka (DFB) kwa kumaliza kileleni mwa Kundi A. Malipo mengine yanayofuata ya kiwango kama hicho ya kiasi cha Euro 50,000 yatalipwa tena ikiwa tu timu hiyo itafanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali. Pesa hizo zinatarajiwa kuongezaka hadi Euro 400,000 ambayo kila mchezaji atapokea kama wakiweza kulishinda taji la Kombe la Ulaya ikiwa wao ndio wenyeji wa mashaindano hayo.
Malipo yatakuwa yanaongezeka.
Malipo hayo yanafanyika kulingana na matokeo ya timu hiyo uwanjani na kama Ujerumani wangefungwa dhidi ya Uswisi basi wasingeweza kuyapokea malipo hayo hata kama tayari walikuwa wamefanuikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora.
Soma zaidi. Ujerumani yaibamiza Scotland 5-1 mchezo wa ufunguzi EURO 2024
Mwaka 2021 , wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani hawakupokea bonasi kwenye mashindano ya Euro waliposhika nafasi ya pili kwenye kundi lao na vivyo hivyo baada ya kutolewa katika hatua ya makundi kwenye mashindano ya kombe ka dunia 2022 nchini Qatar.
Pesa ya zawadi ni jumla ya Euro milioni 331 na imegawanywa kulingana na ushiriki na matokeo ya uwanjani. Shirikisho la Soka la Ujerumani DFB wanatazamiwa kupokea milioni 13.25 baada ya kushinda kundi lao na kutinga hatua ya 16 bora ingawa kutakuwa na ongezeko la pesa kulingana na kila hatua ya mashindano na kama timu hiyo itakuwa ikipata ushindi.
Dpa.