1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Wabunge wa Thailand kumchagua Waziri Mkuu mpya

16 Agosti 2024

Wabunge wa Thailand wanapiga kura hii leo ya ikiwa wanaweza kumteua Paetongtarn Shinawatra kuwa Waziri Mkuu mpya wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4jWst
Thailand | Paetongtarn Shinawatra
Paetongtarn Shinawatra ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Pheu Thai anatarajiwa kuchaguliwa na bunge kuwa Waziri Mkuu mpya Picha: Matt Hunt/NurPhoto/picture alliance

Paetongtarn mwenye miaka 37 ambaye baba na shangazi yake pia walikuwa mawaziri wakuu huenda akawa kiongozi mdogo kabisa katika historia ya Thailand ikiwa atachaguliwa.

Kura hiyo inayotarajiwa kupigwa saa nne kwa majira ya Thailand inafuatia uamuzi wa mahakama ya juu nchini humo kumundoa madarakani Waziri Mkuu Srettha Thavisin baada ya kumchagua waziri anayekabiliwa na makosa ya uhalifu.

Atalazimika kupigiwa kura 247 za bunge hilo lenye jumla ya vita 493.