1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Mwanawe Shinawatra ateuliwa kugombea uwaziri mkuu Thailand

15 Agosti 2024

Chama tawala nchini Thailand Pheu Thai Party kimetangaza Alhamisi kumteua Paetongtarn Shinawatra, mwenye umri wa miaka 37 kama mgombea wake wa kiti cha waziri mkuu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jWDl
Paetongtarn Shinawatra, mwenye umri wa miaka 37 ateuliwa kama mgombea wa chama tawala wa kiti cha waziri mkuu
Paetongtarn Shinawatra, mwenye umri wa miaka 37 ateuliwa kama mgombea wa chama tawala wa kiti cha waziri mkuu Picha: Matt Hunt/NurPhoto/picture alliance

Tangazo hili linatolewa siku moja baada ya mahakama kumuondoa waziri mkuu aliyekuwa madarakani Srettha Thavisin kufuatia kesi ya maadili iliyofunguliwa dhidi yake.

Wabunge hapo kesho Ijumaa, watapiga kura kuamua iwapo watamuidhinisha Paetongtarn kama waziri mkuu. Chama cha Pheu Thai ndicho kilicho na wingi bungeni na ndicho chama kikubwa katika muungano wa vyama tawala ulio na jumla ya vyama 11 nchini humo. Srettha ndiye waziri mkuu wa tatu wa chama hicho kuondolewa madarakani na Mahakama ya Katiba na anaondoka afisini baada ya kuhudumu chini ya mwaka mmoja.