SiasaThailand
Mahakama ya Thailand yamuondoa Waziri Mkuu madarakani
15 Agosti 2024Matangazo
Wiki iliyopita mahakama hiyo iliagiza chama kikuu cha upinzani kuvunjwa.
Mahakama ya Katiba ilitoa uamuzi huo kufuatia madai dhidi ya Srettha ya kumteua waziri aliyefungwa jela kwa tuhuma za kutaka kumhonga afisa wa mahakama.
Mahakama hiyo ilipiga kura 5 dhidi ya 4 na kuagiza Srettha kuondoka madarakani mara moja.
Baraza la Mawaziri litaendelea na shughuli zake chini ya serikali ya mpito hadi Bunge litakapomuidhinisha Waziri Mkuu mpya.
Kura ya Bunge ilipangwa kufanyika siku ya Ijumaa lakini hakuna ukomo wa wa muda wa kujaza nafasi hiyo.
Srettha amesema muda mfupi baada ya hukumu hiyo kwamba anaheshimu maamuzi na kwamba alipenda kuheshimu maadili wakati wote wa uongozi wake.