Waasi wauwa 15 mashariki mwa Kongo
19 Aprili 2024Vyanzo vilivyotowa ripoti vimelituhumu kundi la waasi la CODECO ambalo linadai kutetea maslahi ya watu wa kabila la Lendu dhidi ya mahasimu wake wa jamii ya Hema, kwamba limehusika na mauaji hayo.
Soma zaidi: Mapigano yaibuka Kongo kati ya M23 na vijana wazalendo
Kwa mujibu wa Innocent Matukadala, mkuu wa shughuli za utawala wa eneo la Banyali Kalo ambalo linajumuisha vijiji vilivyoshambuliwa, baadhi ya waliouwawa walikuwa wamekatwa viungo.
Ripoti nyingine zilizotolewa na kiongozi wa shirika la kiraia katika eneo hilo, Jean Robert Basiloko, zinasema makundi mawili ya wapiganaji wa CODECO yaliwauwa watu 20 akiwemo chifu wa kijiji kimoja na wanawake watatu na mtoto mmoja.
Vita kwenye eneo hilo viliibuka tena tangu mwaka 2017 ambapo maelfu ya raia wameuwawa na wengine wengi kuachwa bila makaazi.