Waasi wa M23 wa DRC, waudhibiti mji wa kimkakati wa Masisi
6 Januari 2025Serikali ya Kongo na Umoja wa Mataifa wanailaumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuliunga mkono kundi hilo la M23 lakini Rwanda imekuwa inakanusha tuhuma hizo wakati wote. Mapigano yamepamba moto katika wiki za hivi karibuni, na hadi sasa kundi la M23 linaudhibiti mji wa Masisi, ameeleza mbunge wa jimbo hilo Alexis Bahunga. Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa AFC unaoipinga serikali ya Kongo unaojumisha pia kundi la M23 amesema vikosi vya waasi viliingia katikati ya mji wa Masisi tangu siku ya Jumamosi alasiri.Mkuu wa shirika la kimataifa linalofanya kazi katika mji wa Masisi amesema wafanyakazi wa shirika hilo wameshindwa kuendelea na shughuli za kikazi kutokana na maeneo ya biashara kufungwa ambapo imekuwa vigumu kupata au kufikisha bidhaa sehemu zinakohitajika. Mamlaka ya Kongo imesema inachukua hatua za kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo.