Von der Leyen: "Nitapambana na wenye misimamo mikali"
18 Julai 2024Matangazo
Ursula von der Leyen amesema kamwe hatoruhusu watu wenye misimamo mikali kuleta mgawanyiko na kuharibu mtindo wa maisha ya Ulaya.
Ameyasema hayo leo wakati akiomba ridhaa ya wabunge kumpa nafasi ya kuhudumu kwa muhula wa pili kama Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya.
Kiongozi huyo ameliambia bunge la Ulaya, ambalo sasa linajumuisha makundi mawili ya mrengo mkali wa kulia kwamba yuko tayari kufanya kazi na watu wote ili kupambana na itikadi kali za kisiasa.