1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Volker Turk azitaka nchi kuchukua hatua dhidi ya Israel

Idhaa ya Kiswahili9 Septemba 2024

Mkuu wa tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amezitaka nchi kuchukua hatua dhidi ya Israel kufuatia ukiukaji wa sheria za kimataifa.

https://p.dw.com/p/4kQEo
Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesema kwamba kumaliza vita vya karibu mwaka mzima katika Ukanda wa Gaza ni swala la kupewa kipaumbele
Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesema kwamba kumaliza vita vya karibu mwaka mzima katika Ukanda wa Gaza ni swala la kupewa kipaumbelePicha: Kyodo News/IMAGO

Shirika rasmi la habari la Syria SANA, likinukuu chanzo cha matibabu, lilisema idadi ya watu waliokufa kufuatia mashambumubilizi hayo ya Israel imeongezeka na kufikia 14 na wengine 43 kujeruhiwa. Mashambulizi hayo ya anga yamefanyika kwenye jimbo la Hama, katikati mwa Syria. 

Kwa upande wake taasisi ya uchunguzi wa vita vya Syria, iliripoti vifo vya watu 18 wakiwemo wapiganaji wanane wa Syria. Taasisi hiyo imesema mashambulizi makali ya Israel yalifanyika usiku kucha. Imesema mashambulizi hayo yayilenga kituo cha utafiti wa kisayansi huko Masyaf, katika mkoa wa Hama na maeneo mengine na kuharibu majengo na vituo vya kijeshi. 

Iran yaishutumu Israel kwa uhalifu Syria

Rami Abdel Rahman, mkuu wa taasisi hiyo ya kufuatialia vita nchini Syria ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo ni mojawapo ya mashambulizi makali zaidi ya Israel nchini Syria kwa miaka mingi. Hata hivyo, shirika la habari la SANA limesema ulinzi wa anga wa Syria ulidungua baadhi ya makombora ya Israel.

Iran haikusita kulaani mashambulizi hayo ya Israel ambayo iliyaita kuwa ni ya uhalifu. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Nasser Kanani amezitaka nchi za magharibi kuacha kuipa silaha Israel.

''Nchi hazipaswi kukubali kupuuzwa sheria za kimataifa''

Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi huko Gaza
Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi huko GazaPicha: Ayman Al Hassi/REUTERS

Huko mjini, Geneva Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema kumaliza vita vya karibu mwaka mzima huko Gaza ni kipaumbele kwa ulimwengu. Turk amezitaka nchi kuchukua hatua katika kile alichokiita hatua ya Israel ya

kupuuza waziwazi kwa sheria ya kimataifa katika uvamizi wa maeneo ya Palestina.

"Nchi hazipaswi na haziwezi kukubali kupuuzwa kwa wazi sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya lazima ya Baraza la Usalama na amri za Mahakama ya Kimataifa ya Haki.", alisema Turk. 

Netanyahu alaani kitendo cha ''ugaidi''

Katika tukio jingine, dereva wa lori mwenye asili ya Jordan aliwapiga risasi na kuwaua walinzi watatu wa Israel katika kivuko cha mpaka kati ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Jordan, jana Jumapili, kabla ya kuuawa na jeshi la Israel. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alilaani tukio hilo na kumshutumu mshambuliaji huyo kama gaidi.

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema leo kwamba limeyashambulia maeneo kadhaa ya kusini mwa Lebanon ambayo yameaminika kuwa ngome ya kundi la Hezbollah.

Vyanzo: AFP, Reuters, DPA