1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Hamas wasema, Netanyahu akwamisha mapatano

5 Septemba 2024

Kundi la Hamas limemlaumu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kujaribu kuzuia makubaliano ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4kIiG
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: OHAD ZWIGENBERG/AFP

Hii ni baada ya Benjamin Netanyahu kusema Hamas ndio waliokataa kila kitu kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano.

Lawama kutoka kila upande zimejitokeza wakati ambapo Netanyahu anakabiliwa na shinikizo la kufikia makubaliano na kuwezesha kuachiwa kwa mateka waliobakia.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Israel ilitangaza vifo vya mateka sita waliokutwa wamekufa ndani ya tobwe moja la Gaza.

Hamas wanaitaka Israel iondoke kabisa Ukanda wa Gaza.

Wamesema hakuna haja ya makubaliano mapya kwa sababu walishaukubali mpango wa kusimamisha mapigano uliopendekezwa na Rais Biden miezi kadhaa iliyopita.

Wizara ya mambo ya nje ya Qatar nchi ambayo ni mpatanishi mkuu imesema mtazamo wa Israeli utasababisha kufifia kwa juhudi za amani.