SiasaKorea Kusini
Yoon na Kishida wahofia ushirika wa Urusi na Korea Kaskazini
11 Julai 2024Matangazo
Taarifa kutoka ofisi ya Yoon mapema leo imesema viongozi hao wawili wanaohudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya NATO, kwa mwaka wa tatu mfululizo, walikutana pembezoni na kujadiliana wasiwasi huo, mjini Washington siku ya Jumanne.
Tangu kuingia madarakani mwaka 2022, Yoon amejaribu kurekebisha uhusiano na Tokyo ulioathiriwa na mivutano ya kihistoria iliyoanzia na ukaliaji wa Japan nchini Korea kati ya mwaka 1910 hadi 1945.
Seoul na Washington wamekuwa wakiishutumu Korea Kaskazini kwa kuipatia silaha Urusi inazotumia kuishambulia Ukraine.