1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Putin kusaini makubaliano ya ushirikiano na Korea Kaskazini

18 Juni 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameahidi kujenga mifumo mbadala ya biashara na usalama na Korea Kaskazini ambayo haidhibitiwi na mataifa ya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4hAzj
Russischer Präsident Wladimir Putin und Nordkoreas Machthaber Kim Jong Un
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (kushoto) wakisalimiana wakati wa mkutano wao kwenye Ukumbi wa Vostochny Cosmodrome mnamo Septemba 13, 2023.Picha: Vladimir Smirnov/AFP

Katika barua iliyochapishwa na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini kuelekea ziara yake nchini humo, Putin pia ameiahidi Pyongyang msaada usio na shaka.

Kiongozi huyo wa Urusi amesema nchi hizo mbili zimeimarisha uhusiano mzuri katika kipindi cha miaka 70, uliobuniwa kwa misingi ya usawa, kuheshimiana na uaminifu.

Soma pia: Korea Kaskazini yakanusha kubadilishana silaha na Urusi 

Putin ameishukuru Korea Kaskazini kwa kuiunga mkono Urusi katika "oparesheni yake maalum ya kijeshi" nchini Ukraine.

Barua hiyo imechapishwa siku moja baada ya nchi hizo mbili kutangaza kuwa Putin ataitembelea Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 24 kuanzia leo Jumanne.

Mshauri wa sera za kigeni wa Putin Yuri Ushakov amesema Urusi na Korea Kaskazini huenda zikatia saini makubaliano ya ushirikiano wakati wa ziara hiyo yatakayojumuisha masuala ya usalama.