1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Kenya na Haiti wakutana Nairobi

11 Oktoba 2024

Viongozi wa Kenya na Haiti wametowa mwito kwa washirika wao wa kimataifa kutimiza ahadi walizotowa kwa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4lhLi
Kenia | UN Friedensmission in Haiti
Picha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Viongozi hao wamesema ujumbe huo unahitaji rasilimali zaidi na kwamba bajeti yake itamalizika Machi mwaka 2025. Umoja wa Mataifa uliahidi kutoka dola milioni 85 kuusaidia ujumbe huo, lakini umetowa milioni 68 mpaka sasa.

Rais William Ruto, aliyekutana Nairobi na Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille amesema nchi yake itapeleka askari 600 zaidi mwezi Ujao.

Kenya ambayo inaongoza ujumbe huo wa kumaliza vurugu zinazosababishwa na magenge, imepeleka takriban maafisa 400 nchini Haiti wanaoshirikiana na wanajeshi na polisi kutoka Jamaica.

Nchi zilizoahidi kuchangia wanajeshi, ikiwemo Chad, Benin, Bangladesh na Barbados zimeshindwa kuchukua hatua hiyo hadi sasa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW