Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waijadili DRC
1 Desemba 2024Matangazo
Viongozi hao waliokutana Jumamosi bado walishindwa kupiga hatua kufuatia kutokuwepo kwa rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo na kuondoka mapema kwa mwenzake wa Rwanda katika mkutano huo wa kilele wa kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Taarifa iliyosomwa mwishoni mwa mkutano huo wa faragha mjini Arusha ilisema tu kwamba kuna haja ya kuzijumuisha pamoja juhudi zote za kutafuta amani ya kudumu Mashariki mwa Kongo. Rais Paul Kagame aliondoka muda mfupi baada ya mkutano huo lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kutoshiriki kwa Felix Tshisekedi. Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Salva Kiir wa Sudan,Samia Suluhu wa Tanzania,William Ruto wa Kenya,Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.