Viongozi wa G7 waapa uungaji mkono zaidi kwa Ukraine
25 Februari 2024Viongozi wa kundi la mataifa tajiri ulimwenguni la G7 wameapa kuendeleza uungaji mkono usioyumba kwa Ukraine, wakati uvamizi wa Urusi ukitimiza miaka miwilisiku ya Jumamosi.
Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano uliofanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa pia na Rais wa Ukraine Volodmry Zelensky, viongozi wa G7 wameitaka Moscow kuondoa kikamilifu na bila masharti vikosi vyake vya kijeshi kutoka eneo linalotambulika kimataifa la Ukraine.
Uvamizi kamili wa Urusi dhidi ya Ukraine ulioamuriwa na Rais Vladimir Putin ulianzishwa mapema Februari 24, mwaka 2022. Vikosi vya Urusi hapo awali vilisonga mbele katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuelekea mji mkuu wa Kiev, lakini vikajielekeza zaidi katika kuyadhibiti maeneo ya mashariki na kusini.
Alichokisema Zelensky: Zelensky asema watashinda vita dhidi ya Urusi, vita vikipindukia mwaka wa tatu
Tangu wakati huo Urusi imeteka majimbo manne mashariki mwa Ukraine kinyume cha sheria.