1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Viongozi wa Afrika watoa wito wa mauzo ya nafaka za Urusi

4 Agosti 2023

Viongozi wa Afrika wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya amani kuhusu Ukraine, wametoa wito wa kufunguliwa kwa mauzo ya nafaka na mbolea ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4UlhG
2nd Russia-Africa Summit: plenary session
Picha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Hatua itakayofufua makubaliano muhimu ya usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi.

Soma pia: Putin asema Urusi iko tayari kurejea katika usafirishaji wa nafakai

Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Vincent Magwenya, amewaeleza waandishi wa habari jana mjini Pretoria kwamba viongozi hao, pia wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ya kuachilia tani laki 200,000 za mbolea ya Urusi iliyozuiwa katika bandari za Umoja wa Ulaya.

Mwezi uliopita, Urusi ilijiondoa kwenye makubaliano yaliyoratibiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia bahari Nyeusi, hatua iliyopandisha bei za nafaka na kuathiri mataifa maskini.

Soma pia: Urusi kuchukua jukumu la kusafirisha nafaka barani Afrika

Wito huo umetolewa wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiishutumu Moscow, kuwa inatumia kujiondoa kwake katika makubaliano kama chambo.