1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Viongozi wa Afrika wahudhuria mkutano na China mjini Beijing

3 Septemba 2024

China imeahidi kuimarisha ushirikiano wa ngazi ya juu na nchi za Afrika kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa pande hizo mbili hapo kesho mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4kEMV
China Peking | Vor China-Afrika Gipfeltreffen
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing, kabla ya mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing, China.Picha: Tingshu Wang/REUTERS

Viongozi wa nchi za Afrika wanatafuta fedha kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu.

China imesema mkutano huo utakuwa tukio muhimu la  kidiplomasia kuliko mingine yote tangu kutokea janga la  maambukizi ya virusi vya Uviko.

China inashika nafasi ya pili kwa nguvu za uchumi duniani, ni mshirika mkuu wa biashara wa bara la Afrika. Biashara kati  pande mbili hizo ilifikia thamani ya dola bilioni 167 mnamo nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Soma pia: Viongozi wa China waahidi msaada zaidi kuchochea uchumi

Mikopo iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika ilifikia kiwango cha juu kabisa mwaka uliopita kulinganisha na miaka mitano iliyopita. Baadhi ya viongozi wa Afrika wameshawasili mjini Beijing.

Vyombo vya habari vya China vimeripoti kwamba Rais wa China Xi Jinping amekutana na rais wa Kenya William Ruto.