1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani, UK zadungua droni na makombora ya Wahouthi

10 Januari 2024

Vikosi vya Marekani na Uingereza vimezitungua droni zaidi ya 20 na makombora matatu yaliyovurumishwa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuelekea njia za kimataifa za meli katika bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4b3FQ
Meli ya kivita ya Marekani | USS Carney
Meli ya kivita ya Marekani USS Carney ikifyatua kombora la kuharibu droniPicha: U.S. Navy photo/abaca/picture alliance

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM imesema katika taarifa yake kwamba waasi hao wamefanya shambulizi kubwa la makombora dhidi ya meli kutoka maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen kuelekea kusini mwa bahari ya Shamu.

Soma pia: Waziri wa ulinzi wa Israel awaonya Wahouthi

Kamandi ya CENTCOM imesema droni na makombora hayo yameangushwa na ndege za kivita aina ya F/A -18 zinazoendesha shughuli zake kutoka kwenye manuwari ya kivitia ya Marekani ya USS Dwight D. Eissenhower na meli moja ya kivita ya Uingereza na tatu za Marekani.