1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Israel awaonya Wahouthi

21 Desemba 2023

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant amewaonya Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya kufanya mashambulizi zaidi katika bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4aQoI
Israel Tel Aviv 2023 | Joav Galant
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav GallantPicha: Abir Sultan/AP Photo/picture alliance

Waziri Gallant amesema Israel haitavumilia vitisho dhidi ya taifa hilo. Gallant aliyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye kituo cha jeshi la wanamaji karibu na mji wa Eilat kwenye pwani ya bahari ya Shamu.

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema ikiwa Wahouthi wataendelea kufanya uchokozi, kwa kujaribu kuushambulia mji wa Eilat kwa makombora au kwa namna nyingine yoyote, Israel itajua la kufanya.

Matumaini ya kusitishwa mapigano Gaza yaongezeka

Amesema majeshi ya Israel yapo tayari kwa lolote. Waziri huyo wa ulinzi wa Israel ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kiongozi wa Wahouthi Abdel Malek al-Houthi kuzitaka nchi kutojihusisha na mfungamano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani wa kuilinda bahari ya Shamu kijeshi.