1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Vikosi vya Israel vyaendelea kuishambulia Gaza

31 Januari 2024

Israel imeshambulia maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Ukanda wa Gaza hii leo baada ya kundi la Hamas kusema limepokea na lilikuwa linachunguza pendekezo jipya juu ya usitishaji mapigano na kuwaachiwa kwa mateka Gaza.

https://p.dw.com/p/4bssz
Vikosi vya Israel vikiendeleza oparesheni za kijeshi katika eneo la Khan Younis
Vikosi vya Israel vikiendeleza oparesheni za kijeshi katika eneo la Khan YounisPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Pendekezo hilo lililowasilishwa na wapatanishi baada ya mazungumzo na Israel, lilionekana kuwa mpango madhubuti zaidi wa amani kwa miezi kadhaa katika vita kati ya Israel na Hamas.

Afisa wa juu wa Hamas amesema pendekezo hilo linahusisha mapatano ya hatua tatu ambapo wakati huo kundi hilo litaachia mateka wa kiraia waliosalia, kisha wanajeshi na hatimaye maiti za mateka waliouawa.

Hata hivyo, Wapalestina katika Ukanda wa Gaza wanasema mapatano yoyote yanapaswa kumaliza vita na kuwawezesha kurudi katika nyumba zao.

Vikosi vya Israel vimesema leo kuwa vimeua wapiganaji wasipoungua 25 wa Hamas katika muda wa saa 24 zilizopita, na kwamba wanajeshi wake watatu wameuawa pia katika mapambano.