1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Israel laingia ndani ya mji wa Khan Younis

28 Agosti 2024

Israel imepeleka vifaru ndani ya mji wa Khan Younis kwenye Ukanda wa Gaza na imefanya mashambulio ya kupambana na wapiganaji wa Hamas.

https://p.dw.com/p/4k1Ur
Wapalestina wakirejea mashariki mwa Khan Younis
Wapalestina wakirejea mashariki mwa Khan YounisPicha: Omar Ashtawy/apaimages/IMAGO

Israel imepeleka vifaru ndani ya mji wa Khan Younis kwenye Ukanda wa Gaza na imefanya mashambulio ya kupambana na wapiganaji wa Hamas. Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari, Wapalestina wapatao 34 waliuawa. Wakaazi wa mji huo wamesema vifaru vya Israel viliwashtukiza na kusonga mbele hadi katikati ya mji.

Jeshi la Israel liliwaamrisha watu kuondoka mashariki mwa mji huo wa Khan Younis, lakini watu wengi walikwama wakitafuta mahala salama. Wapalestina, Umoja wa Mataifa na maafisa wa misaada wamelalamika juu ya ukosefu wa maeneo salama.

Hata hivyo, jeshi la Israel limesema lilitoa amri kwa watu kuhama kutoka kwenye maeneo yanayotumiwa na Hamas na wapiganaji wengine kwa ajili ya kufanya mashambulio. Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya kwenye Ukanda wa Gaza, Wapalestina zaidi ya alfu 40 wameshauawa tangu kuanza vita baina ya Hamas na jeshi la Israel.