1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Jeshi la Israel laamuru watu kuondoka kusini mwa Gaza

11 Agosti 2024

Jeshi la Israel leo limewaamuru watu kuondoka kusini mwa Gaza baada ya shambulio baya la anga lililolenga shule moja iliyokuwa inatumika kuwahifadhi watu kaskazini mwa ukanda huo kusababisha vifo vya Wapalestina 80.

https://p.dw.com/p/4jLcq
Gaza Menschen fliehen aus den östlichen Bezirken der Stadt Khan Youni im südlichen Gazastreifen
Kufuatia amri mpya ya kuhama iliyotolewa na jeshi la Israel, maelfu ya watu katika mji wa Khan Younis, wameondoka kuelekea Al Mawasi.Picha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/IMAGO

Israel imesema imelenga kamandi inayotumiwa na kundi la Hamas na kuwaua wapiganaji wasiopungua 19.

Israel imeanzisha tena oparesheni ya kijeshi katika maeneo ambayo awali yaliharibiwa vibaya wakati wa makabiliano na wapiganaji wa Hamas.

Soma pia: Hamas: Shambulizi la Israel kwenye shule liliua watu zaidi ya 100

Idadi kubwa ya wakaazi wa Gaza wapatao milioni 2.3 wamelazimika kuyahama makaazi yao kutokana na vita vya zaidi ya miezi 10 katika ukanda wa Gaza.

Wapalestina wengi wanaishi kwa hofu wakieleza kuwa hakuna sehemu yoyote wanayokimbilia ni salama.