Uwaziri mkuu wa Thuringia bado ni tete
4 Machi 2020Mgombea mwenzake kwenye kinyang'anyiro hicho Bjoern Hoecke wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD akishindwa kupata uungwaji mkono wa bunge.
Ni katika duru ya pili ya uchaguzi wa nafasi ya uwaziri mkuu kwenye jimbo hilo la ThuringiaInes Pohl: Matokeo ya uchaguzi wa Thuringia ni aibu kwa Ujerumani, baada ya jaribio la awali la bunge hilo mapema mwezi Februari kuishia kwenye kashfa baada ya upande wa wabunge wa chama cha Christian Democrat, CDU kuungana na wabunge wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative für Germany, AfD kumuunga mkono mgombea wa nafasi hiyo.
Hatua hiyo ya CDU ililenga kumsaidia mgombea Bodo Ramelow wa siasa za mrengo mkali wa kushoto wa chama cha Die-Linke, kuchaguliwa kwa awamu ya pili katika nafasi hiyo ya uwaziri mkuu.
Chama cha kansela wa Ujerumani, Angela Merkel cha Christian Democratic, CDU awali kilipanga kutoshiriki uchaguzi huo baada ya uchaguzi wa kwanza kukiingiza kwenye mzozo wa kisiasa.
Uamuzi wa wabunge wa CDU kwenye jimbo hilo la Thuringia wa kuvunja kanuni zilizowekwa na chama hicho tawala kuhusu kushirikiana na chama cha AfD cha siasa kali za mrengo wa kulia ulisababisha wimbi kubwa katika sura ya kisiasa kote nchini Ujerumani na hatua ya kushitukiza ya kujiuzulu kiongozi wa chama cha CDU Annegret Kramp-Karrenbauer na kuibua vuta nikuvute ya kimamlaka ndani ya chama hicho.
Ramelow, aliyechaguliwa mwaka 2014 kuongoza jimbo hilo la Ujerumani, alikuwa anahitaji kura nne tu kurejea kwenye wadhifa huo wa uwaziri mkuu wa serikali ya muungano wa vyama vitatu, unaohusisha chama cha Social Democrats cha mrengo wa wastani wa kushoto cha CDU na chama cha walinda mazingira cha Greens.
Lakini kiongozi mpya wa bunge la Thuringia kutoka chama hicho cha CDU Mario Voigt ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba kutoshiriki uchaguzi huu wa leo kunaweza kukaisaidia Thuringia kurejea katika utulivu bila ya kukiuka misingi ya imani ya kisiasa.
CDU pia inapinga kushirikiana na Die Linke na Ramelow pia ameondoa umesema asingependelea kurudi madarakani kwa kusaidiwa na wabunge wa chama cha CDU cha Merkel katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo wa waziri mkuu.
Katika uchaguzi huu Ramelow alitarajia kukabiliwa na changamoto hiyo mpya kutoka kwa Bjoern Hoecke, ambaye chama chake kina viti 22 kwenye bunge la jimbo hilo la Thuringia. Kugombea kwa Hoecke ambaye ni kiongozi wa kundi la siasa kali za mrengo wa kulia la chama hicho linaloitwa Wing, kumeibua maswali kuhusu iwapo mbunge yoyote kutoka chama kingine ataweza kuuunga mkono jaribio lake la kuwa waziri mkuu. Wabunge wanaowaunga mkono wafanyabiashara na Free Democrats wamekataa kuwapigia kura wagombea hao wote Ramelow na Hoecke.
Juu ya hayo yote, kura mpya ya maoni kuhusu Thuringia inaweza ikaongeza wasiwasi ndani ya chama cha CDU katika jaribio lake la kukijenga upya chama hicho baada ya enzi ya Merkel anayetarajiwa kuachia ngazi kabla ya uchaguzi unaofanyika mwakani.
Mashirika: DPAE