1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uswisi kurejesha pesa za ufisadi Kenya

10 Julai 2018

Wakenya wanayasubiri kwa hamu mabilioni ya fedha baada ya serikali ya Uswisi kuahidi kufuata mpango maalumu wa kurejesha fedha  zilizohamishwa katika benki za Uswisi kwa njia za ufisadi.

https://p.dw.com/p/318ES
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) nwa mwenzake wa Uswisi, Alain Berset
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) nwa mwenzake wa Uswisi, Alain Berset Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

J2.10.07.2018-Kenia-Switzerland deal - MP3-Stereo

Haya yamewekwa wazi katika kipindi hiki ambacho rais wa Uswisi Alain Berset yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili. Kutokana na hatua hiyo, DW imezungumza na mchambuzi wa siasa za Kenya aliyeko Nairobi, Profesa Chacha Nyaigoti Chacha, na kwanza kutaka kujua tathimini yake baada ya kuwepo kwa matumaini ya kurejeshwa kwa mabilioni hayo.