1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uswisi bado yaisubiri Kongo ichukuwe fedha za Dikteta Mobutu

26 Juni 2008

Lakini Kongo inaelekea haijali na kimakiwango kidogo cha zusha maswali

https://p.dw.com/p/ERYc
Dikteta Mobutu Sese Seko alipokua katika moja wapo ya nyumba zake za fahari huko Roquebrune-Cap Martin Ufaransa 1996, miezi michache kabla ya kuangushwa madarakani.Picha: dpa

Mahakama ya Uswisi imeamuru franki milioni nane za nchi hiyo zitolewe kwa umma wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-fedaha zilizoko katika akaunti ya

aliyekua kiongozi nchi hiyo hayati Mobutu Sese Seko ilipokua ikijulikana

kama Zaire wakati wa utawala . Waswisi wanajaribu kuishawishi serikali ya Kongo imtume mjumbe maalum kuzipokea fedha hizo kwa niaba ya umma wa nchi hiyo, lakini kiroja cha mambo ni kuwa serikali mjini Kinshasa inaelekea haijali.

Alipoizuru Kinshasa Julai mwaka jana , Rais wa Uswisi Micheline Calm-Rey alimtaka mwenzake Joseph Kabila atume mjumbe maalum kupokea fedha hizo zilizogunduliwa katika akaunti ya Rais wa zamani Mobutu sese Seko 1997. Dikteta huyo aliitawala Kongo wakati huo Zaire kauanzia 1965 hadi 1997.

Alipokua akimaliza ziara yake akiwa katika mkutano na waandishi habari, Rais huyo wa Uswisi alisema hicho ndicho kiasi kilichopatikana-franki milioni 8 sawa na dola milioni 7 na laki 6 za Kimarekani. Ama Rais Kabila alionekana kuvunjwa moyo na akatamka " Kwa bahati mbaya ni franki za uswisi milioni 8 tu ana sio mabilioni niliyoyatarajia." Kutokana na hayo wadadisi wanahisi kiongozi huyo wa Kongo anahisi huu ni mchezo na kulipuuza suala hilo.

André Rothenbuehler kutoka jumuiya isiyochukua faida Aktion Finanzplatz yenye makao makuu mjini Basel na ambayo inaendesha kampeni ya kusaka fedha alizoiba dikteta Mobutu, anasema kwa mujibu wa duru za wizara ya nje ya Uswisi ni kuwa maafisa wa Kongo hawachukuwi hatua kwa sababu ya kuwemo serikalini kwa wafuasi wa Mobutu wakiongozwa na mwanawe wa kiume Nzanga Mobutu ambaye ni waziri wa kilimo. Hivyo uongozi nchini humo hautaki kuvuruga ushirikiano wao katika kugawana madaraka na mtoto wa Mobutu

Kwa mujibu wa Uswisi , haitaki kubakia na fedha hizo muda mrefu, kawa hiyo imeweka muda hadi Desemba 15 mwaka huu na yeyote atakayewasilisha madai atapewa haki yake.

Afisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina alisema mwaka mmoja uliopita walikua na kisa kama hicho kuhusiana na fedha za dikteta wa zamani nchini haiti Jean Claude Duvallier, lakini rais René Préval amechukua hatua za kisheria na kutoa ishara nzito katika kupambana ana rushwa.

Lakini Victor Nzuzi kutoka jumuiya ya Kongo inayopinga madeni Nouvelles Alternatives pour le Dévelopment, yaani njia mbadala kwa ajili ya maendeleo," wanasiasa wa Kongo hawawezi kulikata tawi wanalolikalia." Fedha za Mobutu ni matokeo ya rushwa na wengi wa wanasiasa wa sasa hawakubadilika sana. Pale serikali inapotoa kandarasi kwa Wachina ina maana hongo imelipwa. Kwa kuanza uchunguzi juu ya fedha za Mobutu kunaweza kuzuwa masuali mengi ya kuulizwa.

Jumuiya hiyo ilimuandikia barua mwezi Machi mwanasheria mkuu Mushagalusha kumataka afunguwe kesi juu ya fedha zilizoibiwa na Mobutu, lakini hadi sasa hakufanya hivyo. Bw Nzuzi anajiuliza inakuaje lakini mwanasheria mkuu huyo ameweza kuzuwia akanuti za kiongozi wa upinzani Jean Pierre Bemba ? Bemba aliyeshindana na Kabila katika uchaguzi wa rais 2006 alikamatwa karibu na Brussels Mei 24 mwaka huu, kwa waranti uliotolewa na mahakama ya jinai ya kimataifa. Anashtakiwa kwa makosa mawili ya uhalifu dhidi ya binaadamu na mengine manne ya uhalifu wa kivita. Kiroja cha mambo ni kuwa Bemba ni shemeji yake Nzanga Mobutu- tafauti ni kuwa Nzanga yumo serikalini, Bemba ni mpinzani.