1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usafiri wa reli Ujerumani kuathirika tena siku ya Jumatatu

24 Machi 2023

Ujerumani itakabiliwa na mgomo mwingine wa treni za masafa marefu siku ya Jumatatu, hali inayotarajiwa kuvuruga kwa kiasi kikubwa safari kote nchini humo kutokana na kuahirishwa.

https://p.dw.com/p/4PA48
Deutschland | München Streik Nahverkehr
Picha: Christof Stache/AFP via Getty Images

Mwendeshaji wa usafiri wa reli nchini Ujerumani Deutsche Bahn jana Alhamisi alitangaza kwamba hakutakuwepo treni za masafa marefu siku ya Jumamatu kutokana na mgomo huo.

Uamuzi huo unachukuliwa baada ya muungano wa vyama vya wafanyakazi EVG na Verdi kutangaza mgomo unaolenga kuzorotesha pakubwa mfumo wa usafiri wa umma.

Soma pia: Mgomo wakwamisha maelfu ya abiria Ujerumani

Ujerumani imeshuhudia msururu wa migomo ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali, ambao wanashinikiza kuongezewa malipo ili kukabiliana na mfumuko mkubwa wa bei.