Urusi,Ukraine washindwa kufikia mwafaka huko Uturuki
10 Machi 2022Katika mazungumzo hayo kati ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba yaliofanyika katika mji wa mapumziko wa Uturuki wa Antalya yakiongozwa na mwenyeji wao waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hayakufikia mwafaka wa kusitisha mashambulio kutokana na kile kinachoelezwa kuwa wapo watoa maamuzi katika suala la mzozo wa Ukraine nchini Urusi.
Kuleba ameuambia mkutano huo ambao umeonekana kuwa mgumu kufikia makubaliano kuwa, taifa lake halikujisalimisha, halijajisalimisha wala halitajisalimisha.
Waziri huyo ambae ameonesha nia ya kukutana na mwenzake wa Urusi ameongeza kuwa ujumbe wa Ukraine upo tayari kwa duru nyingine ya mazungumzo ikiwa kuna matarajio na majadiliano ya kina katika kuisaka suluhu.
Soma Zaidi:Urusi na Ukraine zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku nzima
Alisema hakukuwa na ahadi yoyote kutoka kwa mwenzake wa Urusi kuwa watasitisha kufanya mashambulio ili misaada ya kiutu iweze kuwafikia waathirika katika maeneo yaliokumbwa na mashambulio makali ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv.
Kipaumbele kilichotelewa ni kuwahamisha mamia kwa maelfu ya watu waliokwama katika mji uliozingirwa wa mariupol.
Katika mkutano huo Kuleba alimuuliza Lavrov kuwa anaweza kuwasiliana na wenzake waliopo Ukraine ili kusitisha mapigano na kuruhusu njia salama za kufikisha misaada ya kiutu na kutoa uhakikisha wa usalama kwa wahitaji, hatua aliomtaka pia mwenyake afanye hivyo "Nilimuuliza unaweza kufanya hivo? naye hakuji" Kuleba waliwaambia waandishi wa hababri katika mkutano.
Hakuna mwafaka mazungumzo ya Beralus
Wajumbe wa Ukraine na Urusi pia wamekuwa wakikutana huko Belarus, lakini timu iliyotumwa na Urusi kwenye mazungumzo hayo ni ya kawaida, ikikosa mwakilishi kutoka katika baraza la mawaziri la Urusi.
Soma zaidi:Ukraine yasema Urusi inakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda
Katika mkutano unaofanyika Antalya Lavrov alisema mkutano wa leo umethibitisha kwamba muundo wa Urusi na Ukraine huko Belarus hauna mbadala na kudhihirisha kuwa bado rais Putin anayo nia ya kukutana na mwenzake wa Ukraine Volodimry Zelensky.
"katika hili ni muhimu kuweka misingi ambayo inafuata nyendo za kidiplomasia za Belarus." Alisema Lavrov.
Hakukuwa na dalili kwamba walikuwa wamepeana mikono kabla ya kuanza rasmi mkutano huo ambao ulifanyika muda mfupi baada ya shambuliuo dhidi ya hospitali ya watoto katika mji uliozingirwa wa Mariupol huko Ukraine ambapo, watu wasiopungua watatu waliuawa akiwemo mtoto mdogo.
Jumuia ya kimataifa imelaani vikali shambulio hilo.
Urusi:Tunachunguza shutuma, mashambulizi ya hospitali
Urusi imesema kwamba jengo hilo halitumiki tena kama hospitali na ilikuwa chini ya vikosi vya Ukraine.
Katika mkutano na vyombo vya habari muda mfupi baada ya mkutano wa kuisaka suluhu Lavrov ameendelea kukanusha vikosi vya Urusi kufanya shambulio hilo na kuongeza kwamba shambulizi hilo lipo chini ya uchunguzi kwa sasa.
Soma zaidi:Urusi yaongeza mashambulizi katika miji ya Ukraine
Alipoulizwa kama mzozo huo unaweza kusababisha vita vya nyuklia alisema, haamini na hata kuamini kwamba vita vya nyuklia vinaweza kuanza kufuatia mzozo huo, ambao unaendelea kufukuta hadi sasa.