Urusi yatumia kura ya turufu kuisaidia Korea Kaskazini
29 Machi 2024Wataalamu hao hufuatilia vikwazo vya kimataifa vilivyodumu kwa miaka 15 dhidi ya Korea Kaskazini, kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia.
Serikali mjini Seoul imesema inaonyesha wazi kwamba Shirikisho la Urusi, licha ya hadhi yake kama mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limefanya uamuzi usio na uwajibikaji. China imejizuia kupiga kura katika kikao hicho kilichofanyika hapo jana.
Soma pia: Korea Kaskazini ilipeleka makontena 7,000 ya silaha Urusi
Ukraine na Marekani wamelaani pia hatua hiyo ya Urusi ambayo inajiri wiki kadhaa baada ya chombo hicho kusema kinachunguza ripoti zinazodai kuwa Moscow na PyongYang zimekuwa zikibadilishana silaha. Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano huo, Marekani, Ufaransa, Korea Kusini, Japan na Uingereza zimetaja kusikitishwa na matokeo ya kura hiyo.