1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini ilipeleka makontena 7,000 ya silaha Urusi

18 Machi 2024

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Shin Won-sik amesema Korea Kaskazini ilisafirisha makontena 7,000 ya silaha kwenda Urusi kwa ajili ya vita vya taifa hilo dhidi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4drwe
Urusi na Korea Kaskazini ambao ni washirika wa kihistoria zinakabiliwa na vikwazo vingi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Urusi na Korea Kaskazini ambao ni washirika wa kihistoria zinakabiliwa na vikwazo vingi kutoka mataifa mbalimbali duniani.Picha: Yonhap/picture alliance

Waziri huyo wa ulinzi wa Korea Kusini ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa katika mkutano na vyombo vya habari kwamba idadi hiyo inahusu silaha zilizopelekwa Moscow tangu mwezi Julai.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Marekani ilisema silaha zilikuwa njiani kutoka Korea Kaskazini kwenda Urusi, na ilikadiria kuwa Korea Kaskazini imepeleka zaidi ya makontena 1,000 ya silaha za kijeshi nchini Urusi kwa awamu moja.

Urusi na Korea Kaskazini ambao ni washirika wa kihistoria zinakabiliwa na vikwazo vingi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Urusi imewekewa vikwazo kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na Korea Kaskazini imechukuliwa hatua kama hizo kutokana na majaribio yake ya silaha za nyuklia.