1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yaushambulia mji wa bandari wa Odesa huko Ukraine

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Mji wa bandari wa Odesa nchini Ukraine, umekabiliwa na mashambulizi mapya ya makombora ya Urusi mapema leo Jumapili, ikiwa ni muda mchache kabla ya Putin kukutana na Lukashenko.

https://p.dw.com/p/4UHW9
Ukraine-vita- Odessa
Mkaazi mjini Odesa akiwa mbele ya jengo liloloharibiwa na shambulizi la UrusiPicha: Serhii Smolientsev/REUTERS

Mji wa bandari wa Odesa nchini Ukraine, umekabiliwa na mashambulizi mapya ya makombora ya Urusi mapema leo Jumapili. Gavana wa Odesa Oleg Kiper ameandika kupitia mtandao wa Telegram kwamba raia mmoja amepoteza maisha na kutaja raia wengine kuwa wamejeruhiwa. Odesa imekuwa ikishambuliwa mara kwa maratangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

Shambulio hilo limetokea ikiwa ni saa chache kabla ya Rais Vladimir Putin wa Urusi kukutana na mshirika wake mkuu Rais wa Belarus Alexander Lukashenko. Ikulu ya Urusi Kremlin imesema kuwa viongozi hao watakutana mjini Saint Petersburg na wanapanga kujadili ushirikiano na muungano wa kimkakati baina ya nchi hizo mbili.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa marais hao kukutana tangu Lukashenko alipoingilia kati na kusaidia kumaliza uasi uliofanywa na kundi la wapiganaji mamluki la Wagnerla nchini Urusi.