Urusi yaunga mkono hatua za Syria dhidi ya waasi
4 Desemba 2024Matangazo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amesema hii leo kwamba mashambulizi yanayofanywa na waasi katika siku za karibuni yasingewezekana bila ya msaada kutoka nje pamoja na uchochezi.Bila ya kutoa uthibitisho, Zakharova amesema, waasi hao wamesaidiwa ndege zisizotumia rubani na kupewa na mafunzo na mataifa ya kigeni. Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Rais Bashar al-Assad imekuwa ikiisaidia Syria kijeshi tangu mwaka 2015, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Aidha, Zakharova amesema wanawasiliana kwa karibu na Iran na Uturuki kuhusiana na mzozo huo, kufuatia mashambulizi ya kushtukiza ya waasi, ambao wameudhibiti mji wa pili kwa ukubwa wa Aleppo.