Urusi yapiga marufuku vuguvugu la LGBT kwa itikadi kali
1 Desemba 2023Mwelekeo wa kihafidhina wa Urusi uliokuzwa na Rais Vladmir Putin -- ukionesha mara nyingi kama mapambano ya uwepo dhidi ya maadili ya kiliberali ya magharibi-- umeshika kasi tangu uvamizi nchini Ukraine.
Mahakama ya juu imetoa hukumu mjini Moscow siku ya Alhamisi kwa mujibu wa mwandishi wa AFP aliekuwepo mahakamani.
Mahakama haikusema iwapo baadhi ya watu au mashirika yataathirika na hukumu hiyo. Jaji Oleg Nefedov alihukumu kuwa "vuguvugu la kimataifa la umma la LGBT na matawi yake" yalikuwa ya itikadi kali, na kutangaza "marufuku juu ya shughuli zake kwenye ardhi ya Urusi."
Kesi hiyo ilifanyika faraghani na bila kuwepo upande wa utetezi. Chini ya watu 10 walikusanyika nje ya mahakama. "Nilitumai watu zaidi wangekuja (kuonyesha uungaji mkono), lakini ni watu wachache sana waliokuja," alisema mwandishi habari Ada Blakewell.
Soma pia: Mamia ya Waislamu waandamana Kenya kupinga ushoga
"Inaonyeshanamna kila mtu alivyojawa na uoga ... kuzungumzia kitu chochote kinachohusiana na watu wa LGBT."
Jaji alisema amri hiyo inapaswa kutekelezwa mara moja -- ingawa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya kutetea haki yalisema kutakuwa na ucheleweshaji wa urasimu.
Hofu yatawala juu ya watakaoguswa
"Inasababisha mhemko mkubwa, kwa sababu haiko wazi kabisaa nani atashtakiwa chini ya marufuku hii," alisema Noel Shaida, mkuu wa mawasiliano wa shirika la haki za LGBTQ.
Ikiwa itatekelezwa kwa watu binafsi, nembo ya "itikadi kali" inamaanisha, mabaasha, wasagaji na watu waliobadili jinsia wanaoishi Urusi huenda wakabiliwa na vifungo vya miaka kadhaa gerezani.
Shirika la Huma Rights Watch limesema uamuzi huo ulikuwa "unahatarisha aina zozote za harakati za LGBTQ" huku Umoja wa Mataifa ukikosoa hatua hiyo.
Maxim Olenichev, wakili anaefanya kazi na shirika la Pervy Otdel, linalowasaidia waathirika wa ukandamizaji nchini Urusi, alionya juu ya kesi za jinai ili "kuunda mazingira ya hofu."
Marufuku hiyo inamaanisha "ukaguzi kamili na yumkini ugumu katika kutoa msaada, kwa sababu tutalazimika kujificha," alisema Shaida mwenye umri wa miaka 27.
Soma pia: Wanaharakati Uganda wakosoa EU kutochukua hatua dhidi ya sheria ya LGBTQ
Wengi wa wanachama wa timu yake wameondoka Urusi kuratibu msaada kutokea n'gambo kwenye usalama, kama ambavyo imekuwa kwa mashirika mengine ya kutetea haki tangu kuanza kwa uvamizi dhidi ya Ukraine.
Vita vya Ukraine na uchaguzi ujao wa rais 2024
Mwelekeo wa uhafidhina nchini Urusi umeogezeka kasi tangu ikulu ya Kremlin ilipoanzisha uvamizi nchini Ukraine na wakati uchaguzi wa rais wa 2024, ambao unatazamiwa kurefusha utawala wa Putin hadi alau 2030 -- ukikaribia.
Tanya Lokshina, mkurugenzi mshiriki wa Human Rights Watch kanda ya Ulaya na Asia ya Kati, alisema marufuku hiyi "inanuwia kuongeza kisingizio cha watu wa LGBTQ ili kuwavutia wafuasi wahafidhina wa Kremlin kabla ya uchaguzi wa rais wa Machi 2024.
Desemba iliyopita, Putin alitanua sheria ya mwaka 2013 ili kufanya kuwa kosa utataji wowote hadharani wa watu wa LGBTQ au mahusiano yao.
Mnamo Julai mwaka huu wabunge walipiga marufuku uingiliaji wa kitabibu na michakato ya usimamizi inayoruhusu watu kubadili jinsia. Shaida alisema mamlaka zinataka "kubadili nadhari kutoka vita, kushindwa katika vita."
Na mnamo wakati Ikulu ya Kremlin ikichora taswira ya operesheni ya kijeshi nchini Ukraine kama mapambano dhidi ya "uozo wa maadili ya kiliberali", Shaida aliamini Moscow ilipitisha marufuku hiyo ili kujitenga zaidi na mataifa ya Magharibi.
Soma pia: Marekani yaahirisha mkutano wa VVU/UKIMWI nchini Uganda kufuatia sheria tata ya LGBTQ
"Siku moja yataisha lakini kwa sasa tunahitaji kujairibu kuendelea kuishi na kujiokoa," ulisema muungano wa wanawake wanaopinga vita vya Urusi nchini Ukraine, kupitia mitandao ya kijamii kufuatia hukumu hiyo.
Wahafidhina wasifu mabadiliko
Mbunge Pyotr Tolstoy alisema "hili ni tukio la kihistoria, kwa sababu nchi yetu imegusa jambo 'takatifu zaidi' katika ulimwengu wa kiliberali.
Katika mashambulizi yake ya karibuni zaidi kupitia mitandao ya kijamii, Tolstoy aliita LGBT "mradi uliopangiliwa vyema zaidi kudhoofisha jamii za kijadi kutokea ndani."
Kanisa la Orthodox -- linaloongozwana mshirika wa Putin, Kirill -- alikaribisha hatua hiyo.
"Ni aina ya kujilinda kimaadili kwa jamii," alisema Vakhtag Kipshidze, afisa wa Kanisa la Moscow.
Katika eneo lenye Waislamu wengi - linalotawaliwa na Ramzan Kadyrov, anaesema mkoa wake ni wa watu wanaoshiriki ndoa za jinsia tofauti -- pia alisifu hatua hiyo.
"Urusi imeonyesha kwa mara nyingine kwamba si mataifa yote ya magharibi wala Marekani itatunyima jambo muhimu juu ya yote: utambulisho wa kidini na kitaifa," alisema waziri Akhmed Dudaev.