Haki sawaUganda
Wanaharakati Uganda waikosoa EU kufuatia sheria ya LGBTQ
8 Septemba 2023Matangazo
Kwenye taarifa iliyowasilishwa katika bunge la Ulaya siku ya Jumatano, kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ulaya Jutta Urpilainen alisema kuondoa msaada wa kifedha kwa Uganda kutawanyima watu walio katika mazingira magumu msaada muhimu.
Wanaharakati wa haki za binadamu wa Muungano ujulikanao kama Convening for Equality (CFE) walisema kupitia taarifa kwamba msimamo wa Umoja wa Ulaya umeshindwa kuhakikisha fedha zake hazitasaidia dhuluma na ubagudi dhidi ya jamii ya LGBTQ.
Sheria iliyopitishwa dhidi ya vitendo vya ushoga nchini Uganda inatoa adhabu kali ikiwemo uwezekano wa hukumu ya kifo kwa washukiwa.