Urusi yaishutumu N ATO kwa uadui
11 Julai 2023Matangazo
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema nchi yake itachukua hatua zozote kulinda usalama wake.
"Ndio, tunazungumzia juu ya mkutano wa kilele wa NATO, ambao umejikita tu kuijadili Urusi. Urusi inaonekana kama adui, na ndio hasa ajenda yao kuu. Bila shaka, tunaufuatilia, na baada ya hapo tutachukua hatua zinazolenga kuimarisha usalama wetu." Alisema Peskov.
Soma zaidi: Je, Belarus inaelemea wapi zaidi kati ya Urusi na Magharibi?
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema anatarajia kuwa viongozi waliokutana huko Vilnius kutuma ujumbe kwa Ukraine juu ya ombi kuelekea kupata uanachama wa NATO.
Moscow imeelezea kupanuka kwa NATO kuelekea upande wa mashariki kuwa sababu kuu ya uamuzi wake wa kuivamia Ukraine karibu miezi 17 iliyopita.