1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaishambulia miji ya Ukraine kwa makombora

8 Januari 2024

Urusi leo imefanya mashambulizi makali ya makombora kote nchini Ukraine ikiyalenga maeneo ya makaazi na miundombinu ya viwanda mnamo majira ya alfajiri.

https://p.dw.com/p/4ayMU
Uharibifu wa magari katika jengo la gorofa mjini Belgorod unaodaiwa kufanywa na makombora ya Ukraine
Uharibifu wa magari katika jengo la gorofa mjini Belgorod unaodaiwa kufanywa na makombora ya UkrainePicha: REUTERS

Maafisa wa Ukraine kwenye maeneo ya Kryvyi Rih, Zaporizhzhia, Kharkiv, Dnipropetrovsk na Khmelnytskyi wameripoti mashambulizi hayo yaliyohusisha makombora ya kisasa ya Urusi aina ya Kinzhal.

Hadi sasa imethibitika mwanamke mmoja amejeruhiwa huko Kharkiv na viongozi kwenye miji mingine wamesema hasara kamili itabainika baada ya mashambulizi hayo kusitishwa.

Soma pia:  Ukraine: Urusi ilitumia makombora iliyopewa na Korea Kaskazini.

Katika hatua nyingine Urusi imewahamisha karibu wakaazi 300 wa mji wake wa Belgorod ulio karibu na mpya na Ukraine kufuatia kuongezeka mashambulizi yanayaofanya na vikosi vya Ukraine.

Gavana wa mji huo amesema watu hao wamepelekwa kwenye makaazi ya muda yaliyo kwenye wilaya tatu zilizo mbali kidogo na eneo la mpaka.