1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yahofiwa kutoongeza makubaliano ya ngano ya Ukraine

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Kuna wasiwasi iwapo Urusi itakubali kurefusha mkataba wa kusafirisha ngano kutoka Ukraine kutokana na kutoridhishwa kwake na namna makubaliano hayo yanavyoendeshwa, ikishutumu kuvunjwa kwa vipengele kadhaa.

https://p.dw.com/p/4T6XZ
Ukraine I Weizen Export
Picha: Andrew Kravchenko/AP/picture alliance

Mpango wa usafrishaji nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi unaolenga kupunguza mgogoro wa chakula duniani unatazamiwa kumalizika Julai 17.

Umoja wa Mataifa, ambao umeshiriki kupatikana kwa makubaliano hayo, ulisema kwamba mkataba huo una umuhimu mkubwa kwa mamilioni ya watu katika eneo la Pembe ya Afrika, ambao wengine tayari wanakabiliwa na baa la njaa. 

Soma zaidi: Urusi yakubali kurefusha makubaliano ya ngano
Meli ya mwisho ya ngano yaondoka Ukraine

"Kuna idadi kubwa ya nchi ambazo zinategemea ngano ya Ukraine na ikiwa mkataba utavunjika, kutashuhudiwa ongezeko maradufu la bei za vyakula," alisema Afisa Mkuu wa Masuala ya Dharura wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika kanda hiyo, Dominique Ferretti.

Hadi kufikia sasa, Umoja wa Mataifa unasema kiasi cha tani milioni 32.4 zimesafirishwa kutokana na makubaliano hayo.